WAJASIRIA HIPHOP

"Tangazo kwa WAJASIRIA HIPHOP wote wa DSM: Kama unajijua wewe ni mkali au kuna mwana anatisha na anaweza fanya maajabu ndani ya Fidstylefriday... Na pia upo/yupo tayari kuja location j3 ili tushoot show pamoja.. naomba uni/mnitumie Demo/Ngoma zenu humu -----> cheusidawatv@gmail.com ( leo nitazipitia email zenu mie mwenyewe na pia nitawacontact wote mtakaonitumia", FID Q

AFTER XKUL BAAASH


Nyota  wa kwanza kupanda jukwaani alikuwa  ni Rich Mavoko mkali anayemili kihalali singo mpya ya 'One Time' ambaye ki ukweli alipigiwa shangwe za kutosha licha ya kuwa aliifanya shoo hiyo haraka haraka akiwa na ratiba ya kuwahi uwanja wa ndege tayari kwa shoo nyingine  iliyokuwa inamsubiri jijini Mwanza.Badae badae wakafuata wakali wengine kibao ambao hakika walisababisha vya kutosh ana kulifanya eneo lote  la Mbalamwezi  Beach kulipuka kwa shangwe kila msanii alipokuwa kiapanda jukwaani
pengine unaweza kusema kila msanii alifanya Poa sana lakini shukurani za pekee ni kwa mkali Mr Blue ambaye aliafanya vizuri zaidi sambamaba na nyota wengine kama mwana FA, Ommy Dimpoz, Kallah Jeremia, yOUNG d, Makomando, halikadhalika, Bob jUNIOR , Weusi, na bila kuwasahau  waleee Mburula mburula eeeeeeeeee








NENO ‘SKENDO’ LAMTIMUA WEMA KWENYE KIKAO

MALKIA wa tasnia ya filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu amekasirishwa na neno  ‘skendo’ lililotamkwa na mjumbe mmoja katika kikao cha wasanii kilichofanyika katika Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar.

Wema Isaac Sepetu.
Tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita  lilimfanya Wema kuinuka na kupangusa makalio yake kisha kushika hamsini zake akiwaacha wasanii wengine waliokuwa katika kikao hicho wakipigwa na bumbuwazi.
Gazeti la Amani baada ya kuzinyaka taarifa hizo lilimsaka Wema na kumuuliza kulikoni alikimbie neno skendo, naye alikuwa na haya ya kujibu:
“Nani asiyejua kama ninaandikwa sana kwa skendo kwenye magazeti? Sasa mtu anasimama mbele yangu, anatoa hoja kwa kusema ustaa siyo
kuwa na skendo, mbaya zaidi ananitolea macho, sasa unafikiri miye nitatafsiri vipi?” alihoji Wema.
Kama vile haitoshi malkia huyo wa filamu alisema kuwa mzungumzaji alijiandaa kumdhalilisha au alitumwa na watu ili afanye vile kwa makusudi.
“Sikutaka shali ndiyo maana nikaamua kutimua zangu kwa kuwa huwa sipendi ajenda zisizokuwa na kichwa wala miguu,” aliongeza.
Pia, Wema ambaye ni mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006 alisema mzungumzaji aliponda skendo kwa kuwa si staa na hajulikani, laiti angekuwa anajulikana asingeongea utumbo kama aliokuwa akiuongea.
“Huwezi kuwa staa bila ya kuandamwa na skendo na kila sehemu kuna aina yake ya skendo, kwa mfano  siasa ina aina yake ya skendo na michezo halikadhalika, namshangaa yule mbwiga anayetafuta ustaa kupitia majina ya watu,” alisema kwa hasira.


XXL AFTER SCHOOL BASH 2012 at MBALAMWEZI BEACH CLUB


DIAMOND, MARLAW, SHETTA, LINEX, DIMPOZ, SHILOLE, MZEE YUSUF NA WENGINEO KUIPAMBA BIRTHDAY PARTY YA THT DAR LIVE J'PILI HII


‘LAZIMA NIMUUE JACK CHUZ’

MAISHA ya msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ yako hatarini kufuatia ujumbe wa kumuua unaosambazwa na muongoza filamu, Mandela Nicholas ‘Jacob’ anayedai kudhulumiwa na msanii huyo kiasi cha shilingi 325,000.

Kwa mujibu wa ujumbe huo, jamaa huyo amedhamiria kumfanyizia Jack kwa kumcharanga mapanga kisa eti kadhulumiwa kiasi hicho cha fedha ambazo ni malipo ya kumuongozea filamu yake.
Jacob anadai kuwa, awali alimuandikia ‘script’ na kumuongozea filamu msanii huyo lakini kabla kazi haijaisha, wakazinguana hadi kufikishana katika Mahakama ya Mwanzo Ilala jijini Dar.
Hata hivyo, mahakama alimuamuru Jack alipe fedha hizo lakini kinyume chake msanii huyo akawa mgumu kutekeleza, hivyo kwa hasira Jacob akamuandikia Jack sms hiyo ya vitisho.
Sehemu ya ujumbe huo inasomeka hivi; “Labda kifo kiniite leo Jack nitamuua, kama laki 325,000 hajanipa mtasikia. Kama rafiki au ndugu jiandae na mazishi ya marehemu Jk Pentzel full panga tu.”
Sehemu nyingine ya ujumbe huyo ilisomeka hivi; “Wapendwa Jack anachohitaji sasa ni kifo na nitamuua kweli, mimi simsukumi…ila mapanga tu ndiyo dawa yake.
“Utapeli utamuua Jaki, leo kesho, keshokutwa mkisikia msiba ulizia kapigwa panga au? Kama siyo panga siyo Jacob, kama panga na vipande 150 ewaa. Yeye kaburini mimi Segerea. Jasho la mtu haliliwi.”
Akizungumza na mwandishi wetu kuhusiana na sms hiyo, Jack alisema kuwa naye ameipata na katika kujihakikishia usalama wa maisha yake amekwenda kuripoti polisi na kupewa RB.

 


DULLY SYKES- UTAMU


RAY KUTOKA NA WAVES OF SORROW

Msanii wa Bongo Movie almaarufu kama VICENT KIGOSI a.k.a Ray, baada ya kutamba na filamu kadhaa nzuri kama Sister Mary na nyingine kali.
Sasa leo latest info mpya nyingine ambayo tumeipata kutoka kwa msanii huyu ni kwamba anatarajia kuachia filamu yake mpya ambayo inakwenda kwa jina la Wave of Sorrow.

Kwa hiyo kama wewe ni shabiki wa Bongo Movie kaa tayari kwa ujio mwingine kutoka kwa VICENT KIGOSI.

“NAUCHUKIA HUU MWAKA” JOE MAKINI

Msanii wa Hip Hop kutoka A Town City almaarufu kama
JOH MAKINI, baada ya kutamba na ngoma nyingi nzuri hapa Tzee sasa leo baada ya kupiga story na Bk Cop aliweza kufunguka na kusema kwamba mwaka huu ajapata mafanikio yoyote katika kazi zake za muziki.

Lakini anategemea kupata mafanikio mazuri mwaka ujao kwa wewe shabiki wake. Baada ya kufunguka hivyo pia alisema kwamba mwaka ujao ameanda project nzuri kwa ajili ya wewe shabiki wake. @info kamili by JOH MAKINI

MAKAMUA ALIKUWA NA MIPANGO MIZURI MWAKA HUU

Msanii wa Bongo Fleva almaarufu kama MAKAMUA anayetamba na ngoma inayofahamika kwa jina la Don’t Cry, mpaka kupelekea mashabiki kumkubali katika tasnia hii ya muziki hapa Tzee.
Sasa latest info kutoka kwa MAKAMUA ni kwamba leo baada ya kuchonga na Bk cop aliweza kufunguka na kusema alikuwa na ndoto za kufungua band yake pamoja na studio.

Lakini kwa sasa haitowezekana kwa sababu alikuwa anaanda project zake binafsi za muziki lakini alimalizia kwa kusema kwamba mwakani ndiyo ataanza rasmi kupanga mikakati yake ya kufunguka band pamoja na studio yake.

CHRISS BROWN AOMBA RADHI KWA PICHA ALIYOWEKA AKIVUTA MISOKOTO MITATU YA BANGI

Chris Brown amewaomba radhi fans wake kwa picha yake aliyopost kwenye instagram hivi karibuni ikimuonesha akijipeleka higher na marijuana.

‘Don’t wake me up hit maker’ alikuwa criticised sana na watu baada ya ku-upload picha akivuta misokoto mitatu ya marijuana a.k.a weed kwa wakati mmoja alipotembelea kijiwe kimoja cha wavuta bangi na baadae kupiga picha ambazo aliziweka akiwa na marafiki zake wa kijiweni hapo.
reezy ambae alipost picha akiwa katika ziara yake huko Nertherlands, alifunguka kupitia twitter baada ya watu kuponda sana picha hiyo, tweet yake inasomeka “Oh Amsterdam, wote mnani-treat vizuri sana, namuomba radhi kila mmoja ambae alijisikia vibaya kwa picha yangu ya bangi.” Aliandika Breezy .

Akaona kama haitoshi ikabidi atoe na ushauri pia, “naomba radhi kila mtu lakini kama wote hampendi basi msifanye hivyo pia. Ni rahisi.”

Breezy ambae hivi karibuni ameirudia account yake ya twitter baada ya kuitelekeza kwa muda mrefu kwa sababu ya mgogoro wake na mchekeshaji Jenny Johson, hivi karibuni alitweet message ya kwanza akimaanisha he is back again kwenye mtandao huo wa kijamii na anaanza upya, “ Time to start fresh. #newchapter.” Ilitweet Chris Brown.

Mkali huyo wa R&B aliwashauri pia watu wake ‘team Chris Brown’ kutumia vizuri account ya tweeter kwa kusapoti na kuuza muziki wake na sio kuzungumzia mambo ya relationship abuse.

Una chochote cha kusema juu ya habari hii? Weka comment yako hapo chini.

 

MAPRODUCER WAWILI MAARUFU JIJINI ARUSHA WAINGIA KATIKA UGOMVI MZITO

Samtimber Maproducer wawili wakubwa jijini Arusha, Samtimber wa Fnouk Music Studios na Nisher wa Nisher Entertainment wameingia kwenye beef baada ya Samtimber kudai kuwa Nisher amekuwa akimletea dharau.

Akiongea na mwandishi wa habari hii, Samtimber amesema Nisher amekuwa akienda kwenye studio yake wakati akirekodi wasanii na kuanza kumkejeli kuwa anatengeneza ‘Bongo Flava’ na hawezi kufanya mixing.